Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ozil abembelezwa kurudi Ujerumani

Mesu Ozil Ozil abembelezwa kurudi Ujerumani

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo fundi Mesut Ozil yupo kwenye mazungumzo kwa ajili ya kuichezea Ujerumani kwenye michuano ya Kombe la Dunia kwa wachezaji wenye umri zaidi ya miaka 35 itakayofanyika baadae mwaka huu.

Kwa mujibu wa Daily Mail, England itakuwa mwenyeji wa fainali hizo zitakazokuwa na timu nane, ambazo zitafanyika kwenye kipindi cha majira ya kiangazi mwaka huu.

Wenyeji England na Ujerumani zitaungana na mataifa mengine kama Argentina, Brazil, Ufaransa, Italia, Hispania na Uruguay kwenye mikikimikiki hiyo inayofahamika kama Kombe la EPG, linaloandaliwa na Elite Players Group.

Steve McManaman, Thierry Henry na Ronaldinho ni baadhi ya masupastaa wa maana kwenye soka wanaotarajiwa kucheza kwenye michuano hiyo.

Kwa mujibu wa Bild, Ozil anaweza kuitumikia Ujerumani kwenye kombe hilo. Ozil mwenye umri wa miaka 35, mara ya mwisho kuitumikia Ujerumani ilikuwa Kombe la Dunia 2018 kabla ya kutangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya fainali hizo zilizofanyika Russia kumalizika.

Ameripotiwa kuwapo kwenye orodha ya wachezaji sambamba na mshindi mwenzake wa Kombe la Dunia, Sami Khedira.

Nahodha wa Ujerumani kwenye michuano hiyo ya EPG Cup, Kevin Kuranyi amesema: “Mesut Ozil yumo kwenye orodha. Nimeshazungumza naye pia. Lakini, hilo tunajua ugumu wake. Tunajua hali ya siasa na vyombo vya habari ilivyo juu yake. Natumai hilo litafika mwisho na atavaa jezi za Ujerumani.”

Ozil aliwatuhumu viongozi wa chama cha soka cha Ujerumani kuwa wabaguzi baada ya kustaafu soka la kimataifa miaka mitano iliyopita.

Alisema alitengwa baada ya kukutana na Rais wa Uturuki, Recep Erdogan kabla ya fainali za Kombe la Dunia 2018.

Kiungo huyo wa zamani wa Real Madrid na Arsenal alifunga mabao 23 katika mechi 92 alizochezea Ujerunani na alikuwa sehemu ya kikosi cha nchi hiyo kilichonyakua ubingwa wa Kombe la Dunia 2014 huko Brazil.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live