Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ozil, Thierry Henry warudishwa uwanjani

Thiery Henry 14 Ozil, Thierry Henry warudishwa uwanjani

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mastaa wa zamani kwenye soka wakiwemo Ronaldinho, Mesut Ozil, Thierry Henry na Hernan Crespo wanatarajiwa kushiriki michuano mipya ya Kombe la Dunia kwa wachezaji wenye miaka 35 na zaidi, baadaye mwaka huu.

Michuano hiyo mipya itahusisha mataifa nane ambayo yaliwahi kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia miaka iliyopita na itafanyika kwa mara ya kwanza nchini England, mwezi Julai.

Timu za kwanza zilizotajwa kushiriki ni England, Argentina, Brazil, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Hispania na Uruguay.

Mechi saba zinatarajiwa kupigwa kwenye uwanja mmoja ndani ya wiki moja, ingawa bado sehemu itakayotumika haijatajwa, huku taarifa zikisema kuna mazungumzo yanaendelea kufanyika.

Hata hivyo, Kampuni ya EPG, ambayo inasimamia michuano hiyo imeteua manahodha yenyewe ambapo imemtaja Steve McManaman kuiongoza England, Esteban Cambiasso (Argentina), Emerson (Brazil), Christian Karembeu (Ufaransa), Kevin Kuranyi (Ujerumani), Marco Materazzi (Italia), Michel Salgado (Hispania) na Diego Lugano (Uruguay).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live