Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Oviedo mtu wa boli aliyelala selo siku tatu

Boli Tatu Oviedo mtu wa boli aliyelala selo siku tatu

Mon, 19 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

KMC juzi jioni imepambana na kujihakikishia kubaki Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao, baada ya kuinyoa Mbeya City kwa mabao 2-0 na hivyo kushinda kwa jumla ya mabao 3-2 kwenye mechi za play-off na sasa wapinzani wao wataenda kujiuliza kwa Mashujaa ili kusalimiska au kushuka daraja.

KMC ilifungwa 2-1 jijini Mbeya kabla ya kulipa kiasi kwenye Uwanja wa Uhuru na sasa kuwa na uhakika wa kuwepo msimu wa 2023-2024, huku City ikiomba ipenye mbele ya Mashujaa inayowania kupanda daraja kutoka Ligi ya Championship katika mechi mbili zitazopigwa kati ya kesho Jumatatu na Juni 24.

City ikifungwa itaifuta Ruvu Shooting na Polisi kucheza Championship, lakini ikishinda itaizuia Mashujaa kuzipata JKT Tanzania na Kitayosce ziliziopanda moja kwa moja Ligi Kuu Bara.

Lakini nyuma ya mafanikio ya KMC ya kusalimika kushuka daraja kuna beki mtu kazi, Ally Ramadhani 'Oviedo' aliyekuwa miongoni mwa wachezaji walioipandisha timu hiyo daraja mwaka 2018.

Mara baada ya kuipandisha, Oviedo alikaa miezi sita na kutimkia Ihefu FC kwa mkataba wa mwaka mmoja lakini alicheza miezi sita tu na kurudi nyumbani na kukaa nao na hadi juzi alikuwa mmoja ya wachezaji walioipambania isishuke daraja.

Mwanaspoti limepata bahati ya kuzungumza na beki huyo ambaye amezungumza mambo mbalimbali ikiwa nipamoja na tukio baya alilowahi kukutana nalo kwenye maisha yake ya kulazwa selo kwa siku tatu kitatanishi. Kivipi? Endelea naye!

KILICHOMLAZA SELO

Kila mwanadamu ana tukio lake la historia japo inategemea kuna walio na matukio ya furaha, huzuri na wengine matukio ya kuchekesha lakini kwa upande wa beki wa KMC amefunguka tukio la kusikitisha.

"Kwenye maisha yangu ya soka nimekutana na matukio ya kawaida hasa kwa wachezaji wa nafasi ya beki kupata gadi nyekundu au njano hayo ndio matuikio ambayo huwa yanatokea mara kwa mara kwa wanasoka;

"Lakini kwenye maisha yangu ya kawaida nilikutana na tukio la kusikitisha ambalo sitakaa nikalisahau ni siku ambayo nilikaa Oysterbay siku tatu kwa kesi ya kusingiziwiwa." anasema.

Oviedo anasema sababu ya kusoka kituo cha polisi ni kutajwa kuonekana sehemu ya tukio ambayo binti ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini kubakwa huku akiweka wazi kuwa rafiki zake wa karibu na wajomba zake ndio walimtoa.

KIBABAGE FRESHI

Kabla ya Nickson Kibabage kutimkia Siongida Big Stars alikuwa anakipiga KMC sambamba na Oviedo ambaye anathibitisha kuwa hakuwahi kuwa na vita na beki huyo bali kocha ndiye alikuwa anawapa muda wa kucheza kulingana na mechi.

"Sio kweli kwamba tulikuwa na ugomvi tulikuwa tunaelewana kila mmoja alikuwa anatambua ubora wa mwenyeke huku kocha pia akielewa uhitaji wa kila mchezaji kulingana na mechi husika;

"Kibabage ni mchezaji mzuri anavitu ambavyo mimi sina na mimi pia kuna vitu ninavyo yeye hana hivyo kila mmoja alikuwa anahitajika kwa muda husika hatukuwahi kugombana." anasema.

TSHABALALA UFUNDI, KASI

Ni nadra sana kuona mchezaji wa ligi kuu bara anamsifu mchezaji ambaye wanacheza namba moja lakini beki wa KMC, Oviedo amekiri kuwa beki wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kuwa ni mchezaji mzuri ambaye amekuwa akimfuatilia.

“Tshabalala ni beki mzuri mpambanaji anafanya kila kitu uwanjani anapanda kushambulia na kukaba ni mwepesi nimekuwa nikimfuatilia sana na nafurahishwa na uchezaji wake;

“Ni mabeki wengi nawafuatilia lakini nimekuwa nikipendezwa na uchezaji wa Tshabalala najifunza vitu kutoka kwake naamini kuwa mpira ni mchezo wa kujifunza na kumtazama mtu ili kuwa bora.” anasema.

FEDHA ILIVYONG'OA IHEFU

"Nimecheza kwa mafanikio ndani ya KMC pamoja na kutokufanikiwa kuvaa medali hata moja lakini fedha niliyopewa na Ihefu FC ilining'a kwenye timu niliyoitumikia kwa muda mrefu;

"Nilisaini mwaka mmoja Ihefu lakini niliitumikia kwa miezi sita tu na baadae nikarudi tena nyumbani hayo yalikuwa ni makubaliano ya pande zote mbili; "Nilishindwa kuingia kwenye mfumo nilipoenda Ihefu na mara baada ya kurudi tena KMC mambo yangu hayapo vizuri kwani nimekuwa na msimu mbaya." anasema.

Oviedo anasema hana msimu mzuri na timu yake haikuwa na wakati mzuri kutokana na kushindwa kupambana na kukwepana na changamoto ya kushuka daraja wanashukuru Mungu kupata nafasi ya kucheza prayoff.

CHANGANYIKENI HADI KMC

“Nilicheza timu za mtaani tu nimeanza na Bongoyo, Zamaleck, Champion ya kawe baada ya hapo nilienda timu inaitwa Changanyikeni Ranges ipo changanyikeni ilikua inashiriki dalaja la pili hapo ndo nkaanza kujulikana kabla ya kuja KMC;

“Ubora wangu ulianzia mtaani ndio nikaonwa na KMC ambayo naitumikia hadi sasa nilianza kuichezea kabla haijapanda hadi sasa inavyoshiriki ligi kuu pamoja na changamoto kutokuwa na matokeo mazuri lakini ndio timu ambayo imenikuza kiushindani.” anasema beki huyo ambaye anakiri kuwa wazazi wake walikua wanapenda sana asome.

SOKA LIMEMPA TV

Soka limekuwa ajira kwa vijana wenye vipaji na mapenzi ya mchezo wenyewe ambapo vijana wengi wamekuwa wakijiingizia kipato na kuendesha maisha yao.

“Fedha yangu ya kwanza ya usajili nilinunua flat tv na mziki (subuffer) wakati nacheza timu ambayo inashiriki ligi daraja la kwanza, Kwa maisha niliyotoka hadi nilipofikia namshukuru

Mungu bado naendelea kutafuta lakini nilipofika naweza sema mpira umenilipa.” anasema.

Chanzo: Mwanaspoti