Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Out CAFCL; Orlando Pirates walikwenda kushangaa maghirofa Hispania?

Orlando Pirates Wasafisha Kikosi Out CAFCL; Orlando Pirates walikwenda kushangaa maghirofa Hispania?

Sun, 1 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Achana na bejeti kubwa wanayo itumia Orlando Pirates kufanya usajili mkubwa kujiandaa na michuano yote wanayo shiriki kuelekea msimu mpya .

Jana wameondoka mapema katika michuano ya CAF Champions League baada ya kulala mbele ya Jwaneng Galaxy katika changamoto ya Mikwaju ya penalty (5-4) .

Changamoto ya Mikwaju ya penalty ilikuja baada ya Dakika 180 Aggregate kusimama 1-1 .

Wadau wengi wa Soka pale Afrika Kusini wanasema kinacho mwangusha Orlando Pirates ni kununua wachezaji wa kawaida. Unaambiwa ndani ya timu hii kocha akitaka mchezaji chaguo la kwanza katika Kikosi chake atapewa chaguo la tatu Hadi la nne .

Orlando Pirates ni sawa na Kaizer Chiefs Hawa siku zote usajili wao ni wa ujanja ujanja ndiyo maana siku zote pale Kwa Madiba wachezaji wa kiwango Cha juu hutua Sundows.

Kocha wa Jwaneng Galaxy Morena Ramereboli amesema hatukwenda Hispania kuweka kambi lakini tumewaondosha wababe Hawa ambao walikita kambi Hispania.

Mashabiki wengi wa Pirates mara nyingi husema Mamelodi wanabebwa pale PSL lakini wanasahau kwamba Klabu Yao imeachwa mbali sana na Sundows ambayo Ina miliki wachezaji wa kiwango Cha juu .

Mabosi wa Orlando Pirates siku zote hawajawahi kumpa Mwalimu mchezaji wa chaguo la kwanza hata siku Moja kitu kinacho ifanya timu hii iendelee kuwa msindikizaji Kila siku japo kuwa nje ya Uwanja Bado wanapata faida kubwa hasa kwenye biashara ya kuuza jezi na Kusaini mikataba minono kutokana na ukubwa wa jina lao.

Nb Hawa Jwaneng Galaxy siyo wageni Lupaso pale.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live