Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ouma: Ngushi ni mali

Crispin Ngushi Bao 3.jpeg Crispin Ngushi

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha mkuu wa Coastal Union, David Ouma amesema usajili wa Crispin Ngushi kikosini kwake utaongeza kitu pindi Ligi Kuu itakapoendelea Februari.

Ngushi amesajiliwa kwa mkopo kutokea Yanga, akizungumzia usajili wake Ouma amesema ni pendekezo lake na anaushukuru uongozi wa timu hiyo kufanikisha usajili wake huku akisisitiza kuwa atawaofa vitu vingi uwanjani.

“Ngushi anaweza kucheza winga, namba 10 na pia anaweza kukaba, tulikuwa hatuna mchezaji wa aina hiyo kikosini kwetu hivyo kumpata tunatarajia mambo mengi kutokana kwake," amesema Ouma na kuongeza;

“Navutiwa na uchezaji wake nilikuwa nikimfuatilia muda mrefu hata kwenye michuano ya Mapinduzi aliyoyafanya yaliongeza imani kwangu na kuwaomba viongozi waweze kukamilisha usajili wake, nafurahi nipo naye kikosini sasa,”

Akizungumzia usajili mwingine alisema msimu huu wameongeza wachezaji wanne dirisha hili akiwemo mshambuliaji Salum Aiyee huku akiweka wazi kuwa mpango ni kupandisha wengine watano kutoka timu ya vijana.

Alisema wameongeza wachezaji wachache licha ya kuwaacha wengi lengo ni kuona wanakuwa na wachezaji ambao wote watapata nafasi ya kucheza tofauti na msimu uliopita ambao walikuwa na wachezaji wengi na kufikia wakati wengine wameamua kuachana nao wakiwa hawajapata nafasi ya kucheza mechi hata moja.

Chanzo: Mwanaspoti