Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Osimhen aitamani Chelsea mbele ya PSG, Waarabu

Victor Osimhen Chelsea Deal Osimhen aitamani Chelsea mbele ya PSG, Waarabu

Fri, 24 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Straika wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 25, amepanga kukataa ofa za Paris St-Germain na Saudi Arabia ili ajiunge na Chelsea katika dirisha lijalo.

Osimhen anaripotiwa kuwa na ndoto ya kutaka kujiunga na Chelsea kwa muda mrefu na amevutiwa zaidi na ofa yao.

Moja kati ya maeneo ambayo Maurico Pochettino kabla ya kuondoka alisisitiza kwamba anataka yafanyiwe maboresho ni lile la ushambuliaji n jina la Osimhen ndio likawa juu katika orodha ya washambuliaji anaowahitaji.

Licha ya kuondoka kwa Pochettino, Chelsea bado inataka kumsajili Osimhen ingawa ili kufanikisha mchakato huo itatakiwa kuuza baadhi ya wachezaji.

Napoli inahitaji zaidi ya Pauni 100 milioni kwa timu yoyote inayomhitaji lakini lengo la staa huyo ni kutua Chelsea tu na si vinginevyo.

Msimu uliopita Osimhen amecheza mechi 31 za michuano yote na kufunga mabao 17.

KIUNGO wa Manchester City na Ureno Bernardo Silva, 29, ameambiwa kuwa anaweza kuondoka katika dirisha lijalo ikiwa timu zinazomhitaji zikiwasilisha ofa ya walau Pauni 50 milioni.

Silva ambaye ameshinda karibia kila taji kwa ngazi ya klabu, mkataba wake na Man City unamalizika mwaka 2026. Msimu huu amecheza mechi 42 za michuano yote, amefunga mabao 10 na kutoa asisti 11.

MABOSI wa Arsenal wanataka kumsajili golikipa Feyenoord na Uholanzi Justin Bijlow, 26, ili akawe mbadala wa Aaron Ramsdale anayetarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu.

Justin anasajiliwa ili akawe namba mbili mbele ya David Raya anaonekana kutumika zaidi na Mikel Arteta kwa msimu uliopita.

Mkatana wa kipa huyo raia wa Uholanzi unamalizika mwaka 2026.

TOTTENHAM ipo tayari kumuuza mshambuliaji wao Richarlison, 27, katika dirisha lijalo kwa ajili ya kumsajili straika wa Bournemouth, Dominic Solanke, 26.

Richarlison amekuwa akiwindwa na timu za Saudi Arabia tangu kuanza kwa mwaka huu na inaelezwa wanaraka kutoa zaidi ya Pauni 50 milioni kwa ajili ya kumsainisha. Msimu uliopita Solanke amecheza mechi 42 za michuano yote na kufunga mabao 21.

WAWAKILISHI wa kiungo wa Manchester City Kevin de Bruyne wametua Marekani ambako wanafanya mazungumzo na moja ya timu ya Ligi Kuu nchini humo San Diego FC, lakini hadi sasa hakuna makubaliano yaliyofikiwa.

Mbali ya timu za Marekani, De Bruyne pia anahusishwa na baadhi ya timu za Saudi Arabia tangu dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana.

GOLIKIPA wa Everton Jordan Pickford, 30, anaripotiwa kuwaambia watu wake wa karibuni kwamba ataendelea kubakia hapo kwa msimu ujao licha ya Chelsea kuonyesha nia ya kumsajili.

Pickford ambaye alimaliza nafasi yapili nyuma ya David Raya kwenye mchakato wa kuwania tuzo ya kipa bora wa msimu kwa kumaliza na idadi ya mechi chache alizofungwa bao, mkataba wake unamalizika mwaka 2026.

MSHAMBULIAJI wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko, 20, ambaye anawindwa na Chelsea na Atsenal anatarajiwa kufanya maamuzi katika siku chache zijazo ikiwa ataondoka ama kubaki Leipzig.

Timu nyingi zimevutiwa na kiwango alichoonyesha Benjamin kutokana na kiwango bora alichoonyesha kwa msimu uliopita ambapo amefunga mabao 14 katika mechi 42 za michuano yote. Mkataba wake unamalizika mwaka 2028.

NEWCASTLE ipo katika hatua nzuri kwenye mchakato wao wa kupata saini za mabeki wa mawili raia wa England, Tosin Adarabioyo, 26, na Lloyd Kelly, 25, ambao watakuwa huru katika dirisha hili.

Kocha wa Newcastle Eddie Howe amependekeza majina ya mastaa hawa wasajiliwe ili kuboresha eneo lao la ulinzi lililoonekana kuwa na mapungufu makubwa kwa msimu huu.

Chanzo: Mwanaspoti