Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Osimhen, Haller watemwa kikosi bora AFCON 2023

Haller X Osimhen Osimhen, Haller watemwa kikosi bora AFCON 2023

Wed, 14 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya kiwango bora walichoonyesha washambuliaji, Victor Osimhen na Sebastian Haller na kuzisadia timu zao kufika fainali wamekosekana kwenye kikosi bora za michuano ya Afcon 2023.

Osimhen anayekipiga Napoli inayoshiriki Ligi ya Serie A ya Italia amecheza michezo yote tangu hatua ya makundi na kufunga bao moja dhidi Guinea ya Ikweta huku akiatarajiwa angefunga mabao mengi kwenye fainali hizo.

Haller anayekipiga Borussia Dortmund aliipa Ivory Coast ubingwa kwa mabao yake mawili, licha ya kuanza kucheza hatua ya 16 bora dhidi ya Senegal, akifunga kwenye nusu fainali dhidi ya Congo na fainali dhidi ya Nigeria.

Haller alikosena kwenye mechi za hatua ya makundi kutokana na kuwa majeruhi kabla ya kurudi hatua ya 16 bora nankuongeza nguvu kikosini.

Kinara wa mabao Emilio Nsue wa Guinea ya Ikweta ndiye anayeongoza kikosi hicho kama mshambuliaji namba moja huku kipa wa Afrika Kusini Ronwen Williams akisimama langoni nchini ya kocha Muivory Coast, Emerse Faé na wote wametwaa tuzo za Afcon 2023.

Tuzo ya kipa bora imeenda kwa Msauzi Ronwen Williams, mfungaji bora Emilio Nsue, mchezaji bora akiwa beki Mnigeria William Troost-Ekong huku kocha bora akiwa ni Emerse Faé.

Kikosi kama ifuatavyo

kipa: Ronwem Williams (Afrika Kusini)

Mabeki:Ola Aina ( Nigeria ), William Troost-Ekong ( Nigeria), Chancel Mbemba (DR Congo), Ghislain Konan (Ivory Coast)

Viungo: Teboho Mokoena (Afrika Kusini), Jean Michael Seri (Ivory Coast), Franck Kessi (Ivory Coast)

Washambuliaji: Yoane Wissa (DR Congo), Emilio Nsue (Guinea ya Ikweta), Ademola Lookman (Nigeria)

Chanzo: Mwanaspoti