Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Oscar Oscar: Katika hili, tunatakiwa kumshukuru Mo

Oscar X Mo Kwa Mo Tulipaswa kushukuru

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakatiu kukiwa na ugumu wa kuwapata Matajiri waliowekeza katika Soka letu kwa lengo la kufanya mahojiano.

Hali ni tofauti kidogo kwa Mwekezaji wa Klabu ya Simba Mohammed Dewji ambae angalau amekuwa akifanya Mahojiano na Vyombo vya Habari.

Licha ya kujitoa kwake, Mo amekuwa akikutana na comment za maudhui tofauti tofauti ambazo si za kufurahisha sasa kutokana na hali hiyo, Mchambuzi wa Michezo kutoka EFM, Oscar Oscar ameandika;

"Ni Matajiri wachache sana wanakubali kuhojiwa. Wengi tungetamani kufanya mahojiano na Rostam Aziz lakini, huwezi mpata kirahisi.

Hawezi kukubali kwa sababu Chochote anachotamka kina Impact kubwa sana kwa Jamii, Serikali na hata Biashara zake binafsi. Wengi tungependa kumuhoji Mzee Saidi Salim Bakhresa lakini, hawezi kukupa fursa hiyo. Mtu kama MO ambaye amekuwa rafiki wa Media tunambeza kweli? Tunamkejeli kweli? This is very unfair!

Kwa wapenzi wa Simba SC ndiyo usiseme kabisa. Pengine MO ndiyo Tajiri anayeongoza kwa kwenda uwanjani na kuvaa Jezi.

Pengine MO ndiyo Tajiri nchini anayejiachia mbele ya timu yake kuliko mwingine yoyote. MO hastahili kubezwa.

Mchezo wa Soka Kwa sehemu kubwa unaonekana ndiyo Starehe ya watu wa Tabaka la chini. Ukiona mtu kama MO anajishusha hadi chini, usimbeze. Ameamua tu kuwa mnyenyekevu. Ukiona MO anakubali kufanya interview, ni jambo la kufurahia na hasa kwa sisi watu wa Media.

Wengi tungetamani kusikia Mzee Bakhresa anasema nini juu ya Azam FC na Soka la Tanzania. Wengi tungetamani kusikia GSM anasema nini juu ya Yanga ijayo na mpira wa Tanzania lakini, tunaishia kuwasikia Wasaidizi wao tu.

MO amekuwa Rafiki mkubwa sana wa Media Kwa Matajiri wa zama hizi za Soka letu lakini ndiyo kwanza tunaishia kumtukana tu mtandaoni! Tunamuona anatafuta KIKI! Tunamuona anataka Trending! Tunamuona anataka sifa!

MO kama Mwanadamu, atakuwa na mapungufu yake kama ilivyo kwako wewe na kwangu mimi lakini kuhusu Media, huyu mtu anatupa heshima kubwa sana. Kutozungumza na Media kwa Matajiri wengine wa mpira wetu, sio sifa.

Sio jambo la kuonekana Mashujaa. Ni kutunyima habari. Ni kutunyima maarifa. Matajiri ambao hawazungumzi na Media hawapaswi kusifiwa kama wengi wanavyodhani. Tunahitaji watu kama MO kwenye Mpira wetu. Tunatamani kumsikia Mzee Bakhresa mwenyewe. Tunatamani kumsikia GSM mwenyewe. MO ni rafiki mkubwa wa Media zetu. Kama hatuwezi kumsifia, basi tumuheshimu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live