Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Oscar Oscar, Baba Levo wamuombea msamaha Manara

Oscar Oscar X Baba Levo Oscar Oscar, Baba Levo wamuombea msamaha Manara

Thu, 8 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watangazaji wa Wasafi FM Oscar na Baba Levo wametokeza hadharani na kumuombea msamaha Msemaji wa Yanga SC na CEO wa Manara TV Haji Manara kwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF Wallace Karia.

Manara amefungiwa na Kamati ya Maadili ya TFF kujihusisha na mpira nje na ndani kwa miaka miwili na sasa kifungo chake kinakwenda ukingoni.

Watangazaji hao kupitia kipindi chao cha JIONI YA LEO wamemuomba Karia amsamehe Manara kwani ni mtu muhimu katika soka la Tanzania.

“ Mzee wangu Karia Manara ni kijana mwenzetu na amekuwa akifanya kazi nzuri Yanga SC na Taifa Stars katika kuuhamasisha mpira. Amefanya kazi kubwa kuhamasisha watu kuupenda mpira wenyewe na sasa biashara imekuwa. Kijana ameteleza na amekuwa mtulivu kukitumikia kifungo chake. Tunakuomba Mzee Karia na kamati zako, umsamehe Haji mpira wetu bado unamuhitaji, kama Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan alivyowaambia Yanga SC wamalizane na Feisal Salum, ndivyo ambavyo tunakuomba Rais Karia kumsamehe Haji “ Oscar Oscar

“ Binafsi hata mimi nimeshawishika kuingia katika mpira kutokana na Haji, hivyo na mimi namuombea radhi asamehewe “ Baba Levo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live