Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Oruma: Job ashukuru hajafungiwa Taifa Stars

Dickson Job Yanga Xd Dickson Nickson Job.

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Wilson Oruma amesema kuwa, beki wa kati wa Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania, Dickson Nickson Job alifanya makosa makubwa kugomea namba kwenye kikosi cha Taifa Stars wakati wa michuano ya AFCOn iliyomalizika nchini Ivory Coast mwezi februari.

Oruma amesema hayo baada ya mchambuzi mwenzake, Jemedari Said kudai kuwa Job hajaitwa kwenye kikosi cha Stars kitakachoenda kwenye michuano ya FIFA Series 2024 huko Azerbaijan hivi karibuni.

Jemedari amesema kuwa Job alikataa kucheza mechi dhidi ya Congo DR ambayo ilikuwa muhimu kwa Taifa Stars mchezo uliochezwa pale Korogho Ivory Coast baada ya Kocha Hemed Morocco kumpanga nafasi ya beki wa pembeni kulia (namba 2), ambapo Job alisema yeye hayuko tayari kucheza namba 2 jambo ambalo lilimlazimu kocha kumpa nafasi hiyo Lusajo Mwaikenda wa Azam.

Kwa upande wake, Wilson Oruma amesema; "Mpaka sasa Dickson Job anachotakiwa kushukuru ni TFF hawajamfungia Kabisa kucheza Taifa Stars.

"Lakini alichokifanya kukataa kucheza mechi muhimu ya AFCON dhidi ya Dkt. Congo huku tayari akiwa ameshachukua posho ambayo ni kutokana na kodi zetu ni usaliti," amesema Oruma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: