Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Orlando Pirates yaanza vyema Soweto Dabi msimu huu 2023/2024

N1SKHPgm.jpeg Orlando Pirates yaanza vyema Soweto Dabi msimu huu 2023/2024

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Timu ya Orlando Pirates inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini (PSL) imepata ushindi wa mabao 1-0 katika mchezo wa Soweto Dabi dhidi ya Kaizer Chiefs, na huu unakuwa ushindi wa kwanza baada ya kucheza Dabi mbili za msimu uliopita bila kupata point tatu.

Licha ya kuwa na umiliki mdogo wa mpira 39-61, mapema dakika ya 20 mshambuliaji Evidence Makgopa aliipatia timu yake ushindi, bao lilidumu ndani ya dakika 90 licha ya kupiga mashuti 4-0 yaliyolenga lango.

Mchezo uliochezwa katika uwanja wa FNB, makocha wote walifanya Sub zote tano kama kanuni za FIFA zinavyoeleza huku Sub ya mapema kabisa ilifanywa na Kocha wa Orlando Pirates dakika ya 7 ya mchezo akitoka mchezaji James Monyane beki wa kulia na kuingia Bandile Shandu ambaye ni kiungo.

Sub zingine zilizofanyika ni zile za dakika za 19' 20' 71' kwa upande wa Kaizer kocha alifanya Sub dakika za 46' 61' 84'.

Huku yakifanyika madhambi mara 13 kwa upande wa Kaizer, 11 kwa upande wa Orlando, Kadi za njano 2 kwa Kaizer, 4 kwa Orlando, Kona 1 kwa Kaizer,3 kwa Orlando.

Kwenye mchezo huu Rais wa Yanga Eng Hersi Said alikuwa mmoja wa walioshuhudia mchezo huo ambapo katika mtandao wa Instagram Hersi alikiri kuwa shabiki wa Kaizer Chiefs

"Kesho (Leo) nitakuwa kwenye Derby ya Soweto kuwaunga mkono Kaizer Chiefs" aliandika

Hata hiyo baada ya mchezo huo katika msimamo wa ligi hiyo Orlando anashika nafasi ya 7 akiwa amecheza mechi 10 na kukusanya pointi 15 juu ya Kaizer Chiefs ambao wanashika nafasi ya 8 wakicheza mechi 12 na kukusanya pointi 14.

Chanzo: Mwanaspoti