Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Opah Clement kutambulishwa Beskitas

Opah Clement Opah Clement kutambulishwa Beskitas

Wed, 8 Mar 2023 Chanzo: dar24.com

Aliyekuwa Mshambuliaji wa Simba Queens Opah Clement leo Jumatano (Machi 08) anatarajiwa kutambulishwa rasmi kwa Mashabiki wa Klabu ya Beskitas inayoshiriki Ligi Kuu Uturuki.

Opah aliondoka nchini jana Jumanne (Machi 07) majira ya Alfajiri na kwenda moja kwa moja Uturuki kwa ajili ya kukamilisha dili hilo la kujiunga na klabu hiyo.

Opah hadi anaondoka nchini alikuwa anaitumikia Klabu ya Simba Queens na ameondoka akiwa ndiye kinara wa mabao kwenye Ligi Kuu ya Wanawake akiwa nayo tisa.

Meneja wa Simba Queens, Seleman Makanya amesema kuwa: “Opah huenda akatambulishwa leo. Kwa sababu jana aliondoka asubuhi na ilitarajiwa mchana awe ameingia.”

Opah, amejiunga na Beskitas kwa mkataba wa miaka miwili. Hii inakuwa mara ya pili kwa Opah kwenda Uturuki kucheza soka, mwaka jana alilijunga na Yikatel Kayseri kwa mkataba wa muda mfupi.

Chanzo: dar24.com