Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Opah Clement auzwa Ulaya

OPAH AUZWA ULAYA Opah Clement auzwa Ulaya

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa klabu ya Simba umefikia makubaliano ya kumuuza nahodha wa Simba Queens, Opah Clement kwenda Besiktas ya Uturuki.

Tayari mshambuliaji huyo kinara ameshaondoka kuelekea nchini Uturuki kwenda kuanza maisha mapya ya soka katika timu yake ya Besiktas.

Mpaka Opah anaondoka Ligi ya Wananawake (Serengeti Lite Womens Premier League) mzunguko wa kwanza umemalizika na yeye ndiye kinara wa ufungaji akiwa amepachika wavuni mabao tisa.

Uongozi wa Simba umemtakia kila lakheri Opah katika majukumu yake hayo mapya na unamkaribisha muda wowote atakapoamua kurejea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live