Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ooh Zinedine Zidane Ooh Pacome Zouzoua

Pacome Shows Ooh Zinedine Zidane Ooh Pacome Zouzoua

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ooh Zidane ulikuwa hekalu la soka, Ooh Pacome wavivu wa kufikiri wanatenda dhambi kukuhesabu wewe ni hekalu, Ooh Zidane ulikuwa mtu aliyekamilika zaidi kwenye wakati wako, Ooh Pacome Nakukumbusha Zidane hajawahi kuumbwa mara mbili. Ooh Mama football asante sana kwa zawadi ya Pacome na Zidane.

Ooh Jua wewe unafahamu zaidi uwezo wa Zidane kuliko sisi kwasababu bila wewe mboni zingeweza kushuhudia binadamu bora, Ooh Mwezi usiku daima unawakilisha ukuu wa Mwenyezi Mungu na pia kutupa ishara kwamba Pacome aliumbwa kwa hesabu tofauti na Zidane. Ooh Jua na Mwezi kamwe hamna deni lolote.

Ooh kifo najua kuna siku utatuchukua lakini huwezi kusahau mema ya miguu wa Zidane, Ooh kaburi wewe ni nyumba ya milele na dhambi za Pacome utasizihesabu pasipo kusahau kuwa na yeye alikuwa mtu kwenye nyakati zake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: