Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Onyango awatuliza mashabiki Simba

Onyango Robertinho 6 Onyango na Kocha Robertinho

Fri, 24 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kati kutoka nchini Kenya Joash Achieng Onyango amesema Wachezaji wa Simba SC wapo tayari kwa mchezo wa Kesho Jumamosi (Februari 25), dhidi ya Mabingwa wa Uganda Vipres SC.

Simba SC itacheza mchezo wa Mzunguuko watatu wa Kundi C, kwenye Uwanja wa St Merry’s nchini Uganda, huku ikikumbuka namna ilivyoshindwa kutamba mbele ya Horoya AC ya Guinea na Raja Casablanca.

Onyango amezungumza na Waandishi wa Habari katika Mkutano Maalum nchini Unganda na kusema: “Vipers ni timu nzuri, tunaiheshimu lakini tumejipanga kikamilifu kuhakikisha tunashinda na kuchukuwa alama zote tatu ugenini”

“Tuna jukumu la kupata matokeo mazuri hapa ili kufanikisha dhamira yetu ya kuiwezesha Simba SC kurudi katika hadhi yake ya ushindani katika michuano hii.”

“Tupo tayari kupambana kwenye mchezo huu, kila mmoja amedhamiria kucheza kwa moyo wake wote ili kuitetea Simba SC, hatukuwa na matokeo mazuri katika michezo miwili, hilo limetupa nafasi ya kujitafakari na kubaini wapi tulipokosea.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live