Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Onyango, Mzamiru, Okrah wapambana Simba SC

Watatu SImba SC Onyango, Mzamiru, Okrah wapambana Simba SC

Mon, 31 Oct 2022 Chanzo: dar24.com

Wachezaji Joash Onyango, Mzamiru Yassin na Augustine Okrah wametajwa kwenye orodha ya wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Oktoba wa Simba SC (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Watatu hao wametajwa kuwania Tuzo hiyo (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month) kupitia Kurasa za Mitandao ya Kijamii za Simba SC leo Jumatatu (Oktoba 31).

Uwezo na Upambanaji waliouonyesha katika Michezo ya Simba SC ya mwezi Oktoba, umewafanya wachezaji hao kuingia kwenye Kinyang’anyiro hicho, ambacho kitaamuliwa kwa kura za Mashabiki na Wanachama zitakazopigwa kupitia Tovuti ya Klabu.

Taarifa iliyotolewa na Simba SC kwenye Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii imeeleza: Wachezaji ambao wanawania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month) mwezi Oktoba ni;

Chanzo: dar24.com