Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Onana azinguliwa na mashabiki

Andre Onana Miss 7 Andre Onana

Mon, 27 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya kusimama vyema katika milingoti mitatu na kuisaidia Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali ya kombe la FA dhidi ya Manchester City, kipa wa timu hiyo Ondre Onana ameshambuliwa kwa maneno ya mashabiki mitandaoni kwa kuruhusu bao moja.

Man United iliyoshinda taji lao la 13 la FA, Jumamosi iliyopita, ilikuwa katika presha ya kupoteza uongozi baada ya Man City kurudisha bao moja lililofunga Jeremy Doku na ubao kusoma 1-2 dakika ya 87.

Mashabiki wanaamini bao hilo la Doku makosa yalikuwa ni ya Onana wakidai alitakiwa aokoe vizuri shuti lililopigwa.

“Haiwezi kuwa mechi ya Man United hadi Onana aruhusu bao, mwingine alisema Onana kaka sisi tumekukosea nini,” waliandika baadhi ya mashabiki kupitia Twitter.

‘Shabiki mwingine aliandika:” nimeangalia marudio ya bao na nimeona lile lilikuwa ni kosa la Onana, nadhani jamaa hana kiwango cha kutosha na sidhani kama atabadilika na kuimarika.”

Onana amekuwa na nyakati ngumu nyingi tangu atue Old Trafford akitokea Inter Milan katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana kwa ada ya Pauni 43 milioni.

Hata hivyo, kipa huyu raia wa Cameroon alionekana kuwa bora katika dakika nyingi za mechi hiyo, akiokoa michomo mitatu ambayo ilikuwa ikienda golini.

Alisajiliwa kuchukua nafasi ya David De Gea ambaye Kocha Erik ten Hag hakuwa anaridhishwa na kiwango chake.

Chanzo: Mwanaspoti