Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Onana atoa neno kutimuliwa Timu ya Taifa Cameroon

Andre Onana Ksl Andre Onana

Wed, 30 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya taarifa kuzagaa kuwa Goli kipa namba moja wa Cameroon Andre Onana, kufukuzwa kwenye timu ya taifa iliyopo Qatar kwaajili ya michuano ya kombe la dunia.

Kipa Huyo ametoa maelezo yake kuhusu tukio hilo huku akiwashukuru mashabiki.

“Nataka kuelezea hisia zangu kwenye nchi na timu ya taifa, jana sikuruhusiwa kuwa uwanjani kuisaidia Cameroon, kama ilivyo kila siku, ili kutimiza malengo, nimeishi kwa nidhamu ili kufikia malengo ya timu”

“Nimejaribu kuweka nguvu zangu zote kutafuta suluhu kama mchezaji anayokutanayo, lakini kwa upande wa pili hawakuwa tayari, matukio mengine ni ngumu kuelezea, ila naheshimu mawazo ya wahusika ili kuleta tija kwenye timu na nchi”.

“Thamani niliyoionesha kama mtu na mchezaji ni moja inayonielezea mimi ni nani, na hiyo ndio familia yangu imenifunza tangu utotoni, kuiwakilisha Cameroon kila mara imekuwa ni fahari. Utaifa kwanza na milele”. Alimaliza kuandika Onana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live