Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Onana asimulia alivyotokea timu za mtaani

Onana App 1024x733 Onana asimulia alivyotokea timu za mtaani

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Willy Onana amesimulia historia ya maisha yake katika soka ambapo anasema alitokea kwenye timu za mtaani.

Akizungumzia kupitia Simba APP, Onana ambaye ameng'aa kwa kutupia magoli huko nchini Uturuki ambako Simba ilikuwa imeweka kambi ya wiki 3, amesema kabla ya kutua Rayon Sports alichezea timu za mtaani kwao, Cameroon.

"Nilitokea timu za mtaani, nikaitwa zile timu za chini ya miaka 17 hapo hapo nikachukuliwa na timu ya Ligi Kuu. Badaa ya hapo, nilikwenda kufanya majaribio Uturuki lakoini hata hivyo nilishindwa kuendelea kwa sababu nilipata majeraha ya mgongo," alisema Onana.

Nyota huyo anasema, alilazimika kurudi nyumbani kwao Cameroon kutibiwa na baadaye ndipo alipojiunga na Rayon ambapo msimu wa kwanza haukuwa mzuri sana lakini wa pili ambao ndio uliopiwa, alifanya vizuri na kuwa MVP wa Rwanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live