Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Onana aingia anga za makipa ghali duniani

Andre Onana Andre Onana

Mon, 24 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester United imetangaza kumsajili kipa mpya, Andre Onana kutoka Inter Milan kwa uhamisho wa Pauni 47 milioni.

Onana, 27, anajiunga na Man United kama kipa chaguo la kwanza baada ya kuachana na David de Gea.

Dili hilo la Old Trafford limemshuhudia Onana - akisaini mkataba wa miaka mitano wenye kipengele cha kuongeza mmoja zaidi iwe sita - huku akiwa kipa ghali namba tatu katika historia ya mchezo wa soka dunaini.

Chelsea ndiyo timu inayomiliki kipa ghali zaidi duniani, wakati ilipolipa Pauni 72 milioni kunasa saini ya Kepa Arrizabalaga, huku Liverpool ikiwa na kipa ghali namba mbili kwenye ulimwengu wa soka baada ya kulipa Pauni 67 milioni kumnasa Alisson - huku wawili hao wote saini zao zilinaswa mwaka 2018 - na sasa Onana anashika namba tatu baada ya kutua Old Trafford.

Onana sasa amemwengua Thibaut Courtois kwenye namba tatu baada ya kunaswa na Real Madrid akitokea Chelsea kwa ada ya Pauni 38 milioni. Kipa wa Manchester City, Ederson anashika namba tano baada ya kunaswa kwa Pauni 35 milioni, huku kipa gwiji kabisa, Gianluigi Buffon uhamisho wake wa Pauni 33 milioni uliofanyika 2001 wakati alipohama kutoka Parma kwenda Juventus unamfanya ashike namba sita.

Alex Meret anashika namba saba baada ya uhamisho wake kugharimu Pauni 32 milioni wakati aliponaswa kutoka Udinese kwenda Napoli mwaka 2018, huku saini mbili za makipa zilizogharimu Pauni 31 milioni kila moja zilizotokea 2019, zikihusisha Barcelona zikishika namba nane na tisa.

Dili hizo ni za Jasper Cillessen kuhamia Valencia na Neto kutua Barcelona, licha ya Neto dili lake la awali lilikuwa Pauni 23.2 milioni kabla ya kuongezeka na kufikia Pauni 31 milioni.

Makipa wa England, Aaron Ramsdale na Jordan Pickford - kila mmoja alinaswa kwa Pauni 30 milioni kutua kwenye timu za Arsenal na Everton mtawalia - makipa hao wanashika namba 10 na 11, wakati kipa ghali wa mwisho, anayeshika namba 12 kwenye orodha hiyo ni Francesco Toldo, aliyenaswa kwa Pauni 25 mil

Man United itatanguliza kulipa Pauni 43 milioni kwenye dili hilo la Onana, kabla ya nyongeza nyingine ambazo zitafanya Mcameroon huyo kutua Old Trafford kufikia Pauni 47 milioni.

Baada ya kukamilisha dili hilo, Onana alisema: "Kujiunga na Manchester United ni heshima kubwa sana na nimefanya kazi ngumu sana kwenye maisha yangu kupata mambo kama haya, nimevuka vikwazo vingi sana.

"Kuingia ndani ya Uwanja wa Old Trafford kwenda kufanya majukumu ya kulinda goli na kusaidia timu ni kitu kingine kitamu. Huu ni mwanzo wa safari mpya kwangu, nikiwa na wachezaji wenzangu wapya na majukumu mapya ya kupambania. Man United ina historia ndefu ya kuwa na makipa mahiri, nitafanya kila kitu kutengeneza heshima yangu hapa kwa miaka mingi ijayo.

"Nafurahia nafasi niliyopata ya kufanya kazi tena na Erik ten Hag na nasubiri kwa hamu kuwa sehemu ya mafanikio kwa sababu nipo tayari kufanya kweli kwenye klabu hii ya aina yake."

Mashabiki wa Man United wanaweza kuonja ladha ya kwanza ya mavitu ya Onana katika mechi wa kirafiki dhidi ya Arsenal leo Jumamosi. Kama atashindwa kucheza kwenye mechi hiyo, basi anaweza kuwapo golini katika mechi ya Borussia Dortmund au Real Madrid. Ujio wa Onana sasa unafungua milango ya Dean Henderson kuhamia jumla Nottingham Forest baada ya ripoti kudai kwamba kipa huyo mwenye umri wa miaka 26 kumtibua Ten Hag mwanzoni mwa msimu ujao. ioni kutoka Fiorentina kwenda Inter Milan mwaka 2001.

MAKIPA GHALI DUNIANI HAWA

1.Kepa Arrizabalaga - Chelsea, Pauni 72milioni 2.Alisson - Liverpoool, Pauni 67milioni 3.Andre Onana - Man United, Pauni 47milioni 4.Thibaut Courtois - Real Madrid, Pauni 38milioni 5.Ederson - Man City, Pauni 35milioni 6.Gianluigi Buffon - Juventus, Pauni 33milioni 7.Alex Meret - Napoli, Pauni 32milioni 8.Jasper Cillessen - Valencia, Pauni 31milioni 9.Neto - Barcelona, Pauni 31milioni 10.Aaron Ramsdale - Arsenal, Pauni 30milioni 11.Jordan Pickford - Everton, Pauni 30milioni 12.Francesco Toldo - Inter Milan, Pauni 25milioni

Chanzo: Mwanaspoti