Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Onana, Skudu wasilete mpira wa kishule

Onana, Skudu Onana, Skudu wasilete mpira wa kishule

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna hawa wachezaji wawili mmoja yuko Simba, Willy Onana na mwingine yuko Yanga, Mahlatse Makudube ‘Skudu’ yuko Yanga hivi mnawafuatilia kweli?

Jamaa kwa kipaji cha kuuchezea mpira Mungu amewajalia hilo wala halifichiki na pengine ndio sababu kubwa iliyochangia timu zao kuwasajili.

Ujio wao ulikuwa gumzo na kila upande ukawa unatamba kwamba wachezaji hao watakomesha mabeki wa timu nyingine kwa chenga na ule udambwi udambwi ambao mashabiki wa soka la bongo tumekuwa tukiuhusudu.

Lakini wakati mwingine anayekukosoa anakusaidia na ana nia nzuri na wewe kuliko yule anayekusifu kila mara hivyo binafsi bora niwaambie ukweli Skudu na Onana ili wachukue tahadharai kabla ya hatari.

Aina ya mpira wanaocheza ni wa kitoto sana na kwa mahitaji ya soka la kisasa, wanaweza kuzigharimu timu zao kwani wamekuwa wakicheza zaidi kwa kulifurahisha jukwaa na sio kutoa mchango mkubwa kusaidia ushindi wa timu lakini pia wapo legelege sana.

Mpira wa kisasa unahitaji mchezaji awe mgumu kwelikweli na acheze zaidi kwa kuisaidia timu badala ya kuendekeza chenga na kuuchezea mpira hata pale ambapo timu inakuwa inajenga shambulizi kwani akifanya hivyo anaweza kuichelewesha kufika haraka langoni mwa mpinzani.

Halafu kingine, wakumbuke kuwa sio kila mchezaji uwanjani atakuwa tayari kuwakaba kistaarabu wakati wanafanya hivyo vitu vyao vya kufurahisha mashabiki jukwaani.

Siku watakutana na mabeki wanaoweka akili zao mfukoni ambao wanaweza kuwachezea rafu mbaya zitakazowaathiri wao na timu zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live