Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Onana, Etoo haziivi

Etoo X Onana Onana, Etoo haziivi

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa shirikisho la soka nchini Cameroon, Samuel Eto’o na nyota wa klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya Cameroon hawaongei tangu fainali za kombe la Dunia za mwaka 2022 zilizofanyika nchini Qatar.

Ugomvi wa Eto’o na Onana ulianza baada ya nyota huyo kuondolewa kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Cameroon wakati wa fainali za kombe la Dunia kitu kilichopelekea Onana kutangaza kustaafu kuitumikia timu hiyo.

Baada ya mashauriano ya muda mrefu Onana alikubali kurejea kuitumikia timu hiyo lakini kilichokuja kuchochea ugomvi wao ni baada ya nyota huyo kuipa kipaombele zaidi klabu ya Manchester United kuliko Taifa lake.

Onana alichelewa kujiunga na kikosi cha timu ya Taifa ya Cameroon kinachoshiriki fainali za mataifa ya Afrika ili aitumikie Manchester United dhidi ya Tottenham Hotspurs.

Mwandishi wa habari za michezo Chris Wheeler amesema,

“Hakuna dalili zinazoonyesha mabadiliko yoyote kwenye ugomvi wa Andre Onana na Rais wa Shirikisho la soka Cameroon Samuel Eto’o”.

“Ni huzuni, hawajaongea tangu fainali za kombe la Dunia zilizofanyika Qatar, na mahusiano yao yamevunjika kabisa”.

“Onana anaweza kurejea Manchester United wiki hii kama Cameroon itaondoshwa kwenye michuano ya AFCON hii leo”.

Cameroon itakipiga hii leo majira ya saa mbili [20:00] usiku dhidi ya Gambia, mchezo huu umebeba hatma ya timu ya Taifa ya Cameroon ya kusonga mbele ama kuondoshwa.

Eto’o baada ya kupoteza mbele ya Senegal alizungumza maneno mazito sana mbele ya wachezaji, akiwaambia hawajitumi kwaajili ya Taifa lao na hawapambani pengine labda kwasababu asilimia kubwa wamezaliwa Ulaya hawana uchungu na Taifa hili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live