Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Omoto aachana na Kariobangi Sharks

Patilah Omoto Patillah Omoto

Thu, 7 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Safari ya miaka 15 ya “Mido Kisheti” Patillah Omoto katika klabu ya Kariobangi Sharks imefikia ukomo kwenye kandanda ya Ligi Kuu nchini Kenya.

Safari ya Omoto, 27, ilianza miongo miwili iliyopita mnamo 2005 baada ya kumwaga wino wa kuitumikia Sharks, lakini mwaka 2013 na 2014 alitoka kwa mkopo na kuenda AFC Leopards pamoja na Bandari FC kabla ya kurejea tena klabuni hapo.

“Ndugu zangu wa Kariobangi Sharks, nashindwa hata namna ya kueleza lakini ningependa kuwaambia najisikia shujaa na mwenye upendeleo kuchezea klabu hii kubwa tangia mechi yangu ya kwanza hapa mwaka 2005″, alisema maneno hayo akiwaaga mashabiki wa timu hiyo.

Kuondoka klabuni hapo hakumaanisha kuwa anatundika daluga bali Omoto anataka kupata changamoto mpya ambapo amesema atatumia kipindi hiki cha mapumziko kutafuta timu mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live