Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Omog kapania Ligi kuu 2021/2022

Omog Mtibwa Kocha mpya wa Mtibwa Sugar, Joseph Omog (kushoto)

Sun, 26 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Klabu ya Mtibwa Sugar umempa mkataba wa miaka miwili kocha Joseph Omong kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho katika msimu mpya wa 2021/22.

Omog, mwenye uraia wa Cameroon, ametua kikosini hapo kwa ajili ya kuchukua mikoba ya kocha Mohammed Badru ambaye mkataba wake ulifika ukingoni.

Ofisa Habari wa timu hiyo, Thobias Kifaru, amesema kuwa tayari wamempatia mkataba kocha huyo kwa ajili ya kukinoa kikosi chao huku wakiwa na matumaini ya kuwa mwalimu huyo atawafikisha katika malengo yao.

“Omog aliwasili hapa Jumatano na tumeshafanya makubaliano yote na kufikia maamuzi ya kumpa mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kukinoa kikosi chetu na nipende kusema kuwa huyu ndio mwalimu wetu rasmi.

“Kupitia kocha huyu nina imani tutaweza kufikia malengo tuliyojiwekea sisi kama timu ambayo ni kuwa katika nafasi za juu za Ligi Kuu Bara kwa msimu huu,” amesema Kifaru.

Kwa upande wake Omog amesema “Nina furaha kurejea tena Tanzania kwa mara nyingine, lakini kwa sasa nikiwa na kikosi cha Mtibwa matarajio yangu ni kufanya vizuri kama nilivyofanya kwenye timu nyingine huko nyuma, kwa usajili ambao umefanyika nina imani tutakwenda kufanya vizuri msimu huu.

“Uongozi umenihakikishia mazingira mazuri ya kazi hivyo ninatarajia makubwa kutoka kwa wachezaji wangu ambapo kupitia wao tutapambana kuiweka Mtibwa kwenye nafasi nzuri.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live