Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Omalla atajwa Azam

Omalla (8).jpeg Omalla atajwa Azam

Sun, 18 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam ipo kwenye mazungumzo na Gor Mahia ya Kenya kwa ajili ya kumpata mshambuliaji, Benson Ochieng Omalla.

Omalla (21) ambaye ni zao la mashindano ya shule yanayofahamika nchini humo kama Chapa Dimba na Safaricom kama ilivyo Umiseta hapa Tanzania anatajwa kuchukua nafasi ya Mzambia, Rodgers Kola.

Katika msimu wake wa kwanza akiwa na Gor Mahia 2020/21, hakupata nafasi ya kucheza sana kwani alianza msimu wa 2021/2022 ambapo alifunga mabao 10 kwenye michezo 15 aliyobahatika kukipiga.

Nyota huyo mbali na kuichezea Gor Mahia ila alienda pia Sweden kucheza soka la kulipwa, lakini alikaa miezi miwili tu kisha akarudi tena nchini Kenya na kumfanya kutimiza msimu wake wa nne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live