Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ollie Watkins anaingia, Darwin Nunez anatoka Liverpool

Watkins X Nunez Ollie Watkins anaingia, Darwin Nunez anatoka Liverpool

Fri, 31 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Aston Villa huenda ikafanya biashara safi na kupiga mkwanja mrefu kwenye mauzo ya mshambuliaji wao Ollie Watkins baada ya kocha mpya wa Liverpool, Arne Slot kuonyesha nia na dhamira ya kumsajili Mwingereza huyo.

Watkins, mwenye mabao 19 kwenye Ligi Kuu England msimu huu aliisaidia Aston Villa kukamatia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, alisaini mkataba mpya wa kubaki Villa Park, Oktoba mwaka jana.

Lakini, sasa Mdachi Slot baada ya kutua Anfield, anamtaka mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 akacheze kwenye kikosi chake baada ya kutokuwa na uhakika wa kubaki na Darwin Nunez, ambaye amekuwa akifukuziwa na Barcelona wakihitaji saini yake kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya.

Nunez hakufunga bao lolote katika mechi 10 za mwisho alizoichezea Liverpool, jambo hilo linamfanya kocha Slot apambane kupata huduma ya Watkins kuja kurithi buti zake.

MANCHESTER United imeripotiwa kuwa na mpango wa kutaka kumtumia mshambuliaji wao, Mason Greenwood kwenye dili la kumsajili supastaa wa Kireno, Joao Felix. Greenwood, 22, alitumikia msimu uliomalizika karibuni kwa mkopo huko kwenye kikosi cha Getafe ya Hispania. Felix aliitumikia Barcelona kwenye msimu uliopita kwa mkopo akitokea Atletico Madrid.

MANCHESTER United na Manchester City zimeripotiwa kuwa kwenye vita kali ya kufukuzia saini ya mshambuliaji wa RB Leipzig, Dani Olmo dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi. Kiungo huyo mshambuliaji (26) amefunga mabao tisa na kuasisti mara tano kwenye mikikimikiki ya Bundesliga msimu huu na amekuwa kwenye rada za timu za Barcelona, Bayern Munich na Liverpool zikihitaji saini yake.

KIUNGO wa Manchester City, Kalvin Phillips amezikaribisha mezani timu za nje ya Ligi Kuu England akitaka kwenda kucheza soka lake ng’ambo ya nchi ya England kwa msimu ujao. Kiungo huyo mambo yake yamekuwa magumu tangu alipotua Man City, akishindwa kuonyesha makali kama alivyokuwa Leeds United, alipowashawishi mabingwa hao wa England kufungua pochi na kunasa saini yake.

ARSENAL ina mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Athletic Bilbao, Nico Williams. Ripoti kutoka London zinafichua miamba hiyo ya Emirates ipo tayari kulipa kiwango kilichotajwa kwenye mkataba wa Willams kwa timu zinazohitaji huduma yake dirisha hili zitatakiwa kulipa ili kumnyakua. Kinachoelezwa ni Williams anaweza kuachana na Bilbao kama italipwa ada ya Pauni 40 milioni.

WINGA wa Kibrazili, Rodrygo Goes amefichua hajui hatima yake kama atabaki Real Madrid zaidi ya msimu huu. Real Madrid ipo kwenye mchakato wa kumsajili Kylian Mbappe, 25, kutoka Paris Saint-Germain kwa uhamisho wa bure jambo linalomfanya Rodrygo ahisi hatapata nafasi ya kucheza mara kwa mara kikosi cha kwanza cha wababe hao wa Santiago Bernabeu.

INTER Milan ina mpango wa kumsajili beki wa kulia wa Manchester United, Aaron Wan-Bissaka dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi Ulaya. Man United imeripotiwa ipo tayari kumpiga bei beki huyo wa kushoto baada ya kuwa na huduma nyingine matata kabisa kwenye nafasi hiyo kutoka kwa Mreno, Diogo Dalot. Kinachoelezwa ni Wan-Bissaka si mzuri sana anapokuwa na mpira.

Crystal Palace imekubaliana na hali halisi hakuna namna zaidi ya kukubali kumpiga bei beki wao, Marc Guehi dirisha hili la uhamisho Ulaya. Beki huyo wa kati amekuwa kivutio kwa klabu nyingi za England, ikiwamo Manchester United. Na uzuri, Palace inatambua mchezaji wao Guehi atahitaji kuhama dirisha hili ili kwenda kujiunga na timu zinazoshiriki michuano ya Ulaya.

Chanzo: Mwanaspoti