Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Olimpiki 2024: Hofu ya Covid yazidi kutanda

Paris Mnara Olimpiki 2024: Hofu ya Covid yazidi kutanda

Fri, 2 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Waandaaji wa michezo ya Olimpiki wameendelea kusisitiza idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona ni ndogo jambo linalopingana na taarifa za ndani kutoka kambi ya wanariadha.

Kwa mujibi wa tovuti ya Reuters, kuna idadi kubwa ya wachezaji wa michezo mbalimbali walioambukizwa virusi hivyo, ingawa baadhi wamesharudi katika hali zao za kawaida.

Baadhi ya wanariadha wanadai hali haijawa sawa katika maeneo wanayokaa na kila uchao wachezaji wanazidi kuambukizwa.

Katika siku za hivi karibuni, Mwogeleaji Adam Peaty ndiye aliyekutwa na virusi hivyo na aligundulika navyo saa chache baada ya kukosa medali ya dhahabu katika shindano la kuogelea umbali wa mita 100.

Mbali ya Adam, Lani Pallister ni mwongeleaji mwingine aliyekutwa na virusi hivyo na ikabidi aondolewe katika na mashindano.

Chanzo: Mwanaspoti