Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ole Gunner Solkjaer ana majibu ?

Ole G Solkjaer Kocha wa Man U, Ole Gunner Solkjaer

Mon, 18 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kipigo kutoka kwa Leicester City siku ya jumamosi ni ishara tosha kuthibitisha kwamba Kocha wa United Ole Gunner Solkjaer ni mtu asie na mipango.

Manchester United ilicheza hovyo na walifundishwa hovyo wakati wakipoteza kwa magoli 4-2 katika uwanja wa King Power.

Ile rekodi ya kucheza mechi nyingi ugenini pasipo kupoteza (29) mbele ya vijana wa Rodgers imefika mwisho.

Bado kulikuwa na makofi kwa Ole Gunnar Solskjaer wakati akienda kushukuru uwepo wao na sapoti yao, licha ya kipigo hicho, Lakini ni kwa muda gani kiwango hafifu kami hiki kinaweza kuvumilika wakati matarajio yakiongezeka ?

Ni takribani miaka mitatu katika wadhifa alionao lakini dalili za awali kabisa mwanzoni mwa msimu huu zinaonesha Manchester United sio miongoni mwa timu zenye uwezo wa kugombea taji la EPL.

Michezo nane mpaka sasa na wako nje ya timu tatu zinazopigiwa upatu , timu ambazo zote zinafundishwa na Makochwa waliowahi kushinda ubingwa wa Ulaya.

Sio suala la bahati mbaya, kiwango kilikua kibaya. Everton wangekua na uwezo wa kushinda Old Trafford, ushindi dhidi ya Wolves haikua halali yetu, hata ushindi wa dakika za lala salama dhidi ya West Ham ulihitaji goli la dakika za mwishoni bila kusahau penati aliyookoa mlinda mlango David de Gea.

Solkjaer haraka alisema inaruhusiwa kwa golikipa wake kufanya saves mara kwa mara lakini tatizo lililopo ndani ya Kikosi cha United, muda mwingine ushujaa wa mtu mmoja hautoshi. De gea alionyesha kiwango bora kwenye mchezo dhidi ya Leicester licha ya kuwa, mwisho wa mchezo alijikuta ameruhusu magoli manne (4).

Mara ya mwisho kwa United kushinda Ubingwa Ligi Kuu ni msimu wa 2012/2013 wakati Kocha akiwa ni Sir Alex Ferguson.

Kabla ya Ole wamepita Makocha kadhaa kama, David Moyes, Luis Van Gaal, Jose Mourinho ambao, baadi yao angalau walishinda baadhi ya vikombe, lakini sio kwa Ole.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live