Aliyekuwa kiungo wa Simba SC, Nelson Okwa amewaomba radhi mashabiki na viongozi wa klabu hiyo iwapo amewaudhi kutokana na kauli yake aliyoitoa baada ya kuondoka klabuni hapo.
Okwa ambaye ni raia wa Nigeria alisema kuwa viongozi wa Simba ndiyo humoangia kikosi kocha na kwamba amepotezewa muda na malengo yake kwa kutopewa nafasi ndani ya kikosi hicho kisha kufungashiwa virago.
"Kipekee sana, ninaomba Msamaha kwa Klabu ya Simba, iwapo Kauli yangu imeumiza watu ingawa sikumaanisha hivyo ilivyotafsiriwa, Sina tatizo ninaitakia Simba sc ifanye vizuri kwenye Michuano yote itakayoshiriki Msimu ujao.
"Nimeona wengi hawataki kuyasema mazuri niliyoyasema, lakini wanaibuka na yale mabaya machache, lakini ni kawaida kwenye Maisha, kila mtu ana uelewa wake.
"Kwa moyo wangu, sitaacha kuishukuru klabu ya Simba, na kipekee msamaha wangu uende kwa Mwenyekiti na ni mtu anaefahamu ninavyomheshimu na kamwe sitaweza kuivunjia heshima Klabu.
"Kwa mara nyingine ninasema asante kwa Klabu ya Simba, na ninaitakia timu kila la heri kwenye mashindano yote," amesema Okwa.