Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Okwa aichambua Yanga

Okwa Nelson 1111 Nelson Okwa

Sun, 6 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kikosi cha Yanga kiliochopo nchini Tunisia kwa pambano la marudiano la mtoano wa kuwania kuingia makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji wao, Club Africain, lakini kiungo mshambuliaji wa Simba kutoka Nigeria ameuchambua mchezo huo wa Jumatano.

Yanga ililazimishwa suluhu na Africain katika mechi ya kwanza iliyopigwa katikati ya wiki hii na sasa inalazimika kusaka sare yoyote ya mabao au ushindi ili irejea rekodi ya mwaka 2016 na 2018 ilipotinga makundi ya michuano hiyo kupitia hatua ya play-off baada ya kutolewa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hata hivyo, wakati Wanayanga wakiwa wapo fifte fifte juu ya timu yao baadhi wakiamini ni kama imeshatolewa na wengine wakijipa moyo huenda ikatoboa, Nelson Okwa wa Simba amevunja ukimya na kuichambua Yanga kabla ya mechi hiyo.

Okwa aliliambia Mwanaspoti, kabla ya kujiunga na Simba aliyokuwa anaifuatilia kupitia mitandao ya kijamii, anaifahamu Yanga kutokana na kukutana nayo kwenye michezo miwili Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita akiwa na Rivers United na kuitoa kwa jumla ya mabao 2-0.

Mnigeria huyo alisema kwa msimu huu Yanga imeonekana kuimarika na kuleta ushindani katika ligi ya ndani ila kwa anga za kimataifa bado sana na inapaswa ijipange upya kwa misimu ujao na sio sasa.

“Kwenye mashindano ya CAF, si rahisi kufanikiwa kwa mara moja, unahitaji kupitia hatua kwa hatua na Yanga lazima ijue haiwezi kwa sasa, kwani hata Simba haikufanikiwa na kuwa kubwa kwa mara moja, walipambana kufika huko,” alisema Okwa na kuongeza;

“Kwa mashindano ya ndani wachezaji wa Simba kabla ya msimu kuanza tumekuwa tukihamasishana wenyewe kwa wenyewe hatutakubali kuona Yanga wanatawala tena.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live