Aliyekuwa Kiungo wa Simba SC, Nelson Okwa ameilalamikia klabu ya Simba kutokuwa na mipango nae tangu akiwa mchezaji wa Kikosi chao.
Okwa ambae ni raia wa Nigeria alijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Rivers United.
Okwa ambae ametangazwa kutemwa na Simba siku chahche zilizoppita anasema;
“Kwenda Ihefu haikuwa kwasababu ya Kiwango changu, nilienda kwa kumuheshimu Kiongozi wangu.
“Kabla sijaenda Ihefu Simba tayari walikuwa wameshavunja mkataba wangu. Walishapeleka barua TFF kuwa mimi sio mchezaji wao tena, sipo tena kwenye list ya wachezaji wao, nilienda Ihefu kukamilisha msimu,” Aliyekuwa mchezaji wa Simba Sc, Nelson Okwa.