Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Oktoba itatoa taswira ya mafanikio ya Simba msimu huu

Kikosi Simba SC 1 1140x640 Oktoba itatoa taswira ya mafanikio ya Simba msimu huu

Sat, 1 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka kupitia vipindi vya michezo vya Global TV na +255 Global Radio, Sistinho wakati akitoa maoni yake kuhusu ratiba ya Simba SC kwa mwezi Oktoba amesema mwezi huu unaenda kutoa taswira halisi ya Simba kimafanikio kwa msimu huu.

“wataufungua mwezi na mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji kesho baada ya hapo wana mechi mikondo miwili ili kuvuka hatua ya awali ya mtoano ya Klabu Bingwa Afrika kwa kuwatoa Premiero De Agosto ndani ya siku 7, baada ya hapo watacheza na washindani wao kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu yaani Yanga SC na Azam FC ndani ya siku 7 nyingine halafu wataufunga mwezi na Mtibwa Sugar.”

“Ukiangalia ni ratiba ambayo inatoa taswira ya msimu kwao kwani, wakiwatoa De Agosto wanaingia katua ya makundi ya Klabu Bingwa ambayo ni msingi wa lengo lao la hatua ya mtoano, na wakipata alama 6 kwenye michezo dhidi ya Yanga SC na Azam FC wanakua wamepunguza makali ya (Tittle Contenders wenzao kwenye ligi ya ndani) washindani wao”

Aidha Sistinho ameendelea kwa kusisitiza kuwa endapo watatolewa na De Agosto kwenye klabu bingwa halafu wakaangusha alama kwenye mechi hizo kubwa itawapunguzia matumaini kwenye msimu huu ambao umeanza na vimbwanga vingi sana Kwenye timu yao hasa kiutawala.

“Mbali na kuwa ratiba hii itatoa taswira yao ya msimu, pia ni kipimo kizuri cha kikosi chao, kama ni kipana au laah, kikosi kipana huweza kuhimili ugumu wa ratiba kama hii.” amesema Sistinho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live