Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Okrah kuikosa robo fainali Mapinduzi Cup

Okrah Amevunjika Pua Augustine Okrah

Sun, 7 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Yanga, Augustino Okra anatarajiwa kuukosa mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya APR unaotarajiwa kuchezwa Januari 7 2024.

Nyota huyo ambaye ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha kwanza alipata maumivu kwenye mchezo wake wa kwanza akiwa na timu hiyo baada ya kugongana na mchezaji wa timu pinzani.

Ilikuwa ni kwenye mchezo dhidi ya KVZ ambapo alikwama kuendelea na mchezo huo baada ya kupata maumivu hayo.

Kocha msaidizi wa Yanga, Mussa Ndaw amesema: "Alikuwepo hospitali kwa siku mbili, sasa amerejea hotelini. Mashabiki watamuona In Shaa Allah nusu fainali au fainali,".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live