Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Okrah atema cheche Simba

Augustine Okrah Oo Okrah atema cheche Simba

Fri, 30 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota wa Simba Mghana, Augustine Okrah amesema bao moja alilofunga wakati kikosi hicho kiliposhinda 3-1 dhidi ya KMC katika mechi ya Ligi Kuu uliopigwa CCM Kirumba Mwanza, Desemba 26, limemuongezea hali ya kujiamini.

Okrah mwenye mabao manne hadi sasa katika ligi, alisema bado hajarejea kwenye ubora ambao watu walitarajia ingawa kitendo cha kufunga kimempa nguvu ya kurudi katika kiwango chake kizuri alichoanza nacho.

“Majeraha ya misuli yaliniumiza kwa kiasi kikubwa kwa sababu kuna baadhi ya michezo niliikosa japo nafurahi kuona nimerudi na kuendelea kuipigania timu yangu, ushirikiano uliopo naamini tutafikia malengo,” alisema Okrah na kuongeza duru la pili ni mgumu kwa vile kila timu imejipanga kuhakikisha inafikia malengo iliyojiwekea, japo kama wachezaji jukumu lao kubwa ni kupambana ili Simba ipate matokeo mazuri.

Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda, alisema urejeo kwa nyota huyo umekuwa muhimu kutokana na kuumia kwa mshambuliaji kinara, Moses Phiri, atakayekuwa nje kwa wiki mbili. “Ratiba inatubana kwa sababu michuano mingi na kila mchezo ni muhimu, hivyo unapomkosa mchezaji mmoja ni pigo” alisema Mgunda.

Chanzo: Mwanaspoti