Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Simba, Augustine Okrah ambaye ni raia wa Ghan amerjea katika klabu yake ya zamani ya Bechem United FC ya nchini kwao.
Taarifa kutoka Ghana zinaeleza kuwa, Okrah ambaye aliachana na Simba mwishoni mwa msimu uliopita kwa makubaliano ya pande zote amesaini mkataba wa mwaka mmoja na amekabidhiwa jezi yake pendwa namba 10.
Okrah alisajiliwa na Simba mwanzoni mwa msimu uliopita na alionyesha kiwango kizuri tangu mwanzo wa msimu wakati akiwafunga wapinzani wao Yanga bao moja kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii licha ya Yanga kushinda mchezo huo.
Baadaye taarifa zilianza kusambaa kuwa mchezaji huyo ana utovu wa nidhamu hivyo akawa anakosa nafasi kwenye kikosi cha Simba, jambo hilo lilisababisha mchezaji huyo kuondoka mwishoni mwa msimu japo Simba hawajawahi kufafanua sababi za kuachana na fundi huyo wa soka.