Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana ambaye anakipiga ndani ya Simba, Okrah amesema kuwa mara baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua sasa yupo tayari kuipambania timu hiyo huku akitamani kukipiga katika mechi dhidi ya Yanga.
Okrah katika mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Yanga alifanikiwa kuifungia Simba bao la kwanza kabla ya Aziz Ki kwa upande wa Yanga kuja kusawazisha kwa mkwaju wa faulo.
Okrah amesema anatamani kupewa jezi na kuiwakilisha Simba katika mchezo huo dhidi ya Yanga akitaka kuwaonyesha mashabiki wa Simba mchango wake mara baada ya kuwa nje kwa muda mrefu.
Simba wanatarajia kuaalika Yanga kwenye dabi ya Kariakoo Aprili 16, 2023 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar.