Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Augustine Okrah na kiungo mkabaji wa timu hiyo, Jonas Mkude, wamereshwa kikosini baada ya kupotea kwa muda.
Viungo hao wameonekana kwenye basi wakiwa Lindi, tayari kabisa kuwakabili Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu utakaochezwa kesho Mei 3, 2023.
Okrah alipotea kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Al Hilal ya Sudan na kukosekana kwenye mechi zote za hatua ya Makundi na Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika.
Mkude yeye amekosekana kwenye baadhi ya mechi hizo kutokana na kutokuwa sehemu ya mipango ya mwalimu wa timu hiyo, Roberto Oliviera 'Robertinho'.