Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Okrah: Haikuwa rahisi kuja Simba

OKRAH Okrah: Haikuwa rahisi kuja Simba

Thu, 14 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji mpya wa Simba SC, Augustine Okrah amefanya mahojiano ya kwanza na Msemaji wa Klabu hiyo Ahmed Ally mara baada ya kutua jijini Dar ambapo ameeleza jinsi ilivyokuwa ngumu kuamua kuichezea Simba.

Amesema, alipoletewa ofa na Simba, alivutana na uongozi wake wakaanza kuvutana lakini mwisho wa siku walikubaliana na uamuzi wake wa kuwachagua Wekundu hao wa Msimbazi.

“Haikuwa rahisi, tulivutana sana na uongozi wangu lakini baadaye walikubaliana na chaguo langu la kuja Simba,” alisema Okrah.

Nyota huyo ametua Msimbazi na kupewa mkataba wa miaka miwili ambapo leo Julai 14, 2022 anatarajia kukwea pipa na wachezaji wenzake kuelekea nchini Misri kwa ajili kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live