Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Okocha: Mo Salah ana presha

Salah AFCON Mohammed Salah

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Gwiji la soka la Afrika, Jay-Jay Okocha amesema hamu ya kupata mafanikio kwenye soka la kimataifa ndicho kitu kinachomfanya supastaa Mohamed Salah kuwa kwenye presha kubwa kuzidi wote Misri.

Mo Salah kwa sasa yupo kwenye kikosi cha Misri kinachoshiriki fainali za Afcon 2023 huko Ivory Coast.

Fowadi huyo amepata mafanikio makubwa kwenye ngazi ya klabu, lakini bado hajashinda taji lolote akiwa na timu ya taifa, akipoteza mara mbili kwenye mechi za fainali za Afcon 2017 na 2022.

Huko Ivory Coast, Misri ilibanwa mbavu na Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa Afcon 2023 na kutoka sare ya mabao 2-2, huku Mo Salah akisawazisha kwa mkwaju wa penalti.

Mechi yao ijayo katika kampeni hiyo ya kujiweka pazuri ili kufuzu hatua ya 16 bora, Misri itakutana na wababe wenzao wa Afrika, Ghana kesho Jumapili, katika mechi ambayo kila upande utahitaji ushindi.

Okocha alisema Misri imekuwa kwenye presha kubwa, lakini wana nafasi kubwa ya kushinda dhidi ya Ghana.

“Misri ni moja ya nchi zinazotarajiwa kushinda ubingwa wa Afcon 2023,” alisema Okocha.

“Mohamed Salah anataka kupata mafanikio kwenye timu ya taifa hivyo presha yote imewekwa kwake. Katika mechi yao ijayo dhidi ya Ghana, wao wana faida kwa sababu wasipopoteza, watakuwa juu yao ya wapinzani wao. Baada ya hapo, Misri itahitaji ushindi dhidi ya Cape Verde ili kufuzu hatua ya 16 bora.”

Okocha alizungumzia pia suala la Mo Salah kucheza kwenye kiungo katika mechi ya Msumbiji badala ya kuwa winga na kocha Rui Vitoria alifanya mabadiliko hayo ya kiuchezaji kwenye dakika za mwisho.

Fundi huyo wa mpira kutoka Nigeria, Okocha amemtaka Mo Salah amwambie kocha wake wa timu ya taifa ni mahali gani anapopaswa kumpanga ili kumpatia matokeo mazuri ndani ya uwanja.

Chanzo: Mwanaspoti