Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Oilers yaichapa Vijana RBA

Rba+pic Oilers yaichapa Vijana RBA

Mon, 20 Jul 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Imani MakongoroOILERS imeiduwaza bingwa mtetezi wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (RBA), timu ya Vijana kwa kipigo cha pointi 75-68.

Katika mchezo huo wa jana Jumapili usiku uliopigwa kwenye Uwanja wa Bandari Kurasini, Oilers ilichomoza na ushindi huo ikiwa ni tofauti ya pointi saba.

Timu hizo zilicheza kwa mtindo wa funga nikufunge, kabla ya Oilers kuwazidi ujanja wapinzani wao dakika za mwishoni na kuchomoza na ushindi huo ambao ni wa pili mfululizo.

Kwa matokeo hayo, Oilers ambayo ilianza ligi vibaya na kufungwa mechi mbili za awali imekamata nafasi ya nane kwenye msimamo ikiwa na pointi sita nyuma ya vinara Kurasini Heat yenye pointi tisa .

Kurasini Heat imecheza mechi tano na kufungwa moja, ABC ni ya pili ikiwa na pointi nane baada ya kushinda mechi nne ilizocheza hadi sasa, JKT ni ya tatu ikiwa na pointi nane katika mechi nne ilizocheza, pointi sawa na za Vijana ambayo hata hivyo imecheza mechi tano na kufungwa mbili.

Mechi nyingine za jana Jumapili, ABC iliwachapa Kurasini Heat pointi 81-63, UDSM Outsiders ikichapwa kwa tofauti ya pointi moja na Mgulani JKT iliyoshinda 61-60.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz