Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ohoo! Onana anataka kuvuruga mambo huko

Andre Onana Sad Ohoo! Onana anataka kuvuruga mambo huko

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa wa Cameroun, Andre Onana, amefunguka baada ya kukosa mechi ya kwanza ya fainali za Afcon 2023 dhidi ya Guinea juzi Jumanne na kudai ana mengi ya kusema.

Simba Wasioshindika walibanwa na kutoka sare ya bao 1-1, katika mechi ambayo Onana hakucheza kwa kuwa alichelewa kujiunga na wenzake baada ya kuitumikia Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham Hotspur, Jumapili iliyopita.

Kukosekana kwa Onana kuliibua mjadala hasa baada ya Cameroon kuangusha pointi kwenye mechi ya kwanza.

Onana alisema: “Nina mengi ya kusema, lakini siwezi kusema hapa kwa sababu tupo kwenye mashindano. Kitu muhimu ni kuwa wamoja. Tupo hapa kushinda Afcon. Nawaomba mashabiki watushabikie kwenye nyakati mbaya na nzuri, nitatimiza majukumu yangu na ndio maana nipo hapa.”

Kipa huyo aliulizwa ni wapi atajitoa zaidi kwenye klabu au timu ya taifa na hapo ndipo aliposema, “ni kama naulizwa nachagua nani, baba yangu au mama yangu, nchi yangu itakuwa ya kwanza, ndio maana nipo hapa.”

Kocha wa Cameroun, Rigobert Song alielezea uamuzi wake wa kumwondoa Onana kwenye kikosi chake katika mechi hiyo ya sare ya 1-1 dhidi ya Guinea, licha ya kipa huyo kusafiri haraka kutoka England hadi huko Yamoussoukro ilikofanyika mechi hiyo.

“Ni kitu kinachoeleweka. Amewasili saa 10 alfajiri. Unataka vipi kucheza?” alisema Song na kuongeza, “Bado ni sehemu ya timu.”

Chanzo: Mwanaspoti