Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ofisi mpya za Klabu ya Yanga zazinduliwa rasmi

Hersi Mwana Fa730 Ofisi mpya za Klabu ya Yanga zazinduliwa

Thu, 8 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uzinduzi wa ofisi mpya za Klabu ya Yanga, umefanyika jana, huku mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma.

Ofisi hizo zilizopo Makao Makuu ya Klabu ya Yanga, Jangwani, zimefanyiwa maboresho makubwa na kuwa za kisasa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Rais wa Klabu ya Yanga, Eng. Hersi Said, alianza kwa kusema: “Kwanza nitoe shukrani zangu kwa Mheshimiwa Hamis Mwinjuma kwa kuitikia wito wetu wa kuja kuzindua ofisi zetu hizi mpya za Jangwani baada ya marekebisho.



“Tunajivunia sana kuwa na jengo ambalo limejengwa kwa ustadi mkubwa likikidhi mahitaji ya uendeshaji wa klabu. Shukrani za kipekee kwa Mzee wetu, Hayati Abeid Karume kwa juitihada zake za ujenzi wa jengo hili. Tunamuombea wetu apumzike kwa Amani na Mwenyezi Mungu akamjaalie kheri.

“Jengo hili limegawanyika maeneo mawili, ambapo zipo ofisi za watendaji mbalimbali wa klabu, na sehemu ya pili ni maalumu kwa ajili ya timu zetu kutumika kama hosteli za wachezaji na viongozi wa benchi la ufundi.

“Eneo hili limebeba historia za mafanikio ya klabu hii. Katika jengo hili pamejaa kumbukumbu kubwa na za kihistoria za klabu hii, ikiwemo mataji, medali na matukio mbalimbali yaliyoshamiri mafanikio makubwa na ya kipekee.

“Jambo kubwa na la kipekee ukifika hapa Jangwani utakutana na mataji ya zamani kabisa ya klabu hii kunyakua ikiwemo mataji ya Taifa Cup, Ligi Kuu na mataji mengine mbalimbali.

“Nisiwe mchoyo wa fadhila kwa Mfadhili na Mdhamini wetu, Ghalib Said Mohamed kwa kutupa hifadhi ya kiofisi kwenye jengo lake kabla ya kufanikisha maboresho ya ofisi zetu.

“Mr Ghalib alifanya kwa nafasi yake kwa kutuhudumia kwa miaka mitatu, sasa ni wajibu wa wanachama wa klabu hii kuhakikisha kuwa ofisi hizi za Jangwani zitaendelea kuimarika na kuwa bora kwa matumizi. Wanachama wa klabu hii wanaalikwa kuja kuhudumiwa ofisi hizi muda wowote.”

Kwa upande wa mgeni rasmi wa shughuli hiyo, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Hamis Mwinjuma, alisema: “Nimekuwa nikipita hapa Jangwani, sijawahi kujua kama kuna shughuli zinaendelea humu ndani. Lakini kwa hili ambalo mmelifanya, kweli ni ishara thabiti ya namna klabu kubwa inavyofanya mambo yake. Nilidhani Injinia (Hersi Said) umekata tamaa lakini kumbe ulikuwa una mpango mkubwa.

“Kiukweli nitakuwa sitendi haki kama sitapongeza juhudi za Mzee wetu Karume kwa hili alilofanya miaka 50 iliyopita. Mzee Karume alikuwa na maono ya mbali kutengeneza mradi mkubwa na wa kisasa ambao leo unakuwa mfano wa kuigwa. Mwenyezi Mungu amrehemu.

“Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia marekebisho ya Mto Msimbazi kupitia Benki ya Dunia, ambapo kutakuwa na mradi mkubwa wa maendeleo katika eneo la Jangwani. Mradi huu utakaofanikisha Klabu ya Yanga kupata eneo lao kutengeneza uwanja wao.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live