Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ofisa Habari wa Dodoma Jiji kujiuzulu kisa Simba

Kikosi Cha Dodoma Jiji 1140x640 Dodoma Jiji

Sat, 1 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ofisa Habari wa Klabu ya Dodoma Jiji, Moses Mpunga amesema hatojihusisha na shughuli za mpira wa miguu iwapo, timu yake itafungwa na Simba SC, kesho.

Amesema, hiyo ni kutokana na ubora na utayari wa wachezaji wao, hivyo Simba SC wakibahatika basi watapata sare.

"Msimu huu tunataka kuzifunga timu zote zinazoshiriki mashindano ya kimataifa, Kwa tulivyojiandaa, tukifungwa na Simba SC, nitaacha kujihusisha na mpira wa miguu," amesema Mpunga.

Ikumbukwe katika misimu yote miwili iliyopita Dodoma jiji FC, haijawahi kuifunga Simba SC, iwe Jamhuri Dodoma au kwa Mkapa Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live