Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ofa za Mayele zawatoa udenda Viongozi Yanga, watachomoa?

Mayele, Lomalisa Moloko Ofa za Mayele zawatoa udenda Viongozi Yanga, watachomoa?

Tue, 11 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashabiki na wapenzi wa Yanga wamekaa mkao wa kula kusikilizia hatma ya straika na Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita na Kombe la Shirikisho Afrika, Fiston Mayele ambaye imeelezwa jana alitarajiwa kukutana tena na mabosi wa Yanga kukata mzizi.

Sasa sikia, kama kuna kitu kinawapasua vichwa mabosi wa Yanga ni ofa za straika huyo zilizopo mezani mwao na kwamba wiki hii inayoanza leo anaweza kuuzwa nje ya nchi kutokana na ofa hizo nono zinazowatoa udenda mabosi hao.

Kwenye meza ya mabosi wa Yanga kuna ofa tatu za fedha nyingi, lakini kubwa ambazo zimeshtua ni zile za Pyramids na Misri na nyingine kutoka Saudi Arabia zinazowapa ugumu mabosi wa Yanga kumbakisha kikosini mshambuliaji huyo.

Iko hivi. Ingawa mabosi wa Yanga wamekuwa wakifanya siri kubwa, lakini uhakika ni kwamba klabu hiyo imepokea ofa ya kufuru ikiwamo ofa ya dola za markani 600, 000 (zaidi ya Sh1.4 Bilioni), huku vurugu za kugombea saini hiyo zikiendelea kwa kasi hatua iliyoongeza presha kubwa kwa mabosi wa klabu.

Yanga inataka kumbakisha Mayele, lakini ofa hizo zinaleta ugumu licha ya mshambuliaji huyo aliyewekwa fedha ndefu na klabu huku akikomalia kutaka aachwe akatafute changamoto mahali pengine baada ya misimu miwili Jangwani.

Endapo Mayele (29) atasimamia msimamo wa kuondoka Yanga anaweza kujikuta anavuna mshahara wa dola 75,000 kwa mwezi (zaidi ya Sh83 milioni), hatua itakayomweka katika ugumu kukubali kusalia klabu hiyo, licha ya mapenzi yake mbele ya timu hiyo.

Kwa mwaka mmoja tu, iwapo atakubaliana na ofa hiyo itamfanya avune jumla ya Dola 900,000 (zaidi ya Sh2.1 bilioni) kiasi ambacho kinampasua kichwa akiomba mabosi wa Yanga kumkubalia ofa hizo ili kama mambo yasipoenda sivyo huko, basi atarudi nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: