Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Odoi aitosa England, kuitumikia Ghana

Odoi Pic Data Callum Hudson-Odoi

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Ghana imefanikiwa rasmi kumshawishi nyota wa Chelsea,  Callum Hudson-Odoi kuitumikia timu ya taifa ya nchi hiyo 'Black Stars' na kuachana na timu ya taifa ya England.

Nyota huyo ametumia vyema kanuni ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ya kuruhusu mchezaji aliyeitumikia timu ya taifa ya wakubwa kwa idadi ya michezo ya kimataifa isiyozidi mitatu, kuitumikia nchi nyingine ya asili.

Taarifa kutoka Ghana zimefichua kuwa winga huyo baada ya kujipa muda mrefu wa kutafakari, ameamua rasmi kukubali kuitumikia Ghana badala ya England ambayo imekuwa haimuiti kikosini.

Uamuzi wa Odoi unadaiwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na kikao chake na kocha mpya mtarajiwa wa Ghana, Chris Hughton ambaye ameanza kwa kuwashawishi nyota wengi wenye asili ya Ghana ambao wanatamba katika Ligi mbalimbali za Ulaya, kukubali kuitumikia timu ya taifa ya nchi hiyo.

Suala la Odoi kukubali kuichezea Ghana lilianza kuonesha dalili za kutimia ndani ya siku za hivi karibuni baada ya nyota huyo mwaka jana kukataa wito wa timu ya taifa ya vijana ya England chini ya umri wa miaka 21 kwa ajili ya mechi ya kuwania kufuzu fainali za Ulaya kwa vijana wa umri huo dhidi ya Czech ambao waliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Mbali na Odoi, Hughton pia amekuwa akimshawishi beki wa kati wa Southampton, Mohammed Salisu ambaye kwa muda mrefu amekuwa akikataa wito wa kuitumikia Ghana.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz