Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Odegaard aipiga mkwara Liverpool

Od Pic Kiungo wa Arsenal Martin Odegaard

Tue, 15 Mar 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo wa Arsenal Martin Odegaard ameionya Liverpool kujipanga kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu England utakaochezwa kesho kwenye uwanja wa Emirates.

Kiungo huyo, 23, alikuwa na mchango mkubwa kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Leicester City, Arsenal ikitoka na ushindi wa mabao 2-0 yaliwekwa kiamiani na Thomas Partey, Alexandre Lacazette aliyefunga kwa mkwaju penalti na kurejea nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Arsenal imepania kulipiza kisasi kwani katika meche yao ya kwanza vijana hao wa Mikel Arteta walipokea kichapo cha mabao 4-0 uwanja wa Anfield, lakini sasa kutokana na kiwango chao bora walichoonyesha hivi karibuni wanaamini mchezo huo hautakuwa rahisi kwa Liverpool.

Odegaard alizungumza kuelekea mchezo huo kupitia kituo cha televisheni cha Sky Sports huku akiwatambia Liverpool ambao wanaifukuzia Manchester City kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England.

“Kila mtu anaamini kwa sababu tumecheza kwa kujiamini sana, muhimu kuendelea kupambana na tusipoteze nguvu, timu yetu ni nzuri yenye uwezo wa kupata matokeo, hautakuwa mchezo rahisi kwa Liverpool hivyo wanatakiwa kujipanga,” amesema Odegaard.

Arteta atakuwa na kibarua kudhihirisha Arsenal ipo imara yenye uwezo wa kushindana na timu kubwa kama Liverpool ambayo moto wa kuotea mbali Ligi Kuu England kwa sasa. Mchambuzi wa soka wa kituo cha televisheni Sky Sports, Jimmy Floyd Hasselbaink amemshindilia Arteta msumari wa moto akidai hiyo itakuwa nafasi kwake kuonyesha Arsenal imefika mbali kwa kiasi gani. “Walianza msimu kwa kusuasua sana, lakini sasa Arsenal imeimarika, jambo kubwa wamepambana, mechi ya kesho itakuwa mtihani kwao kudhihirisha hili, itaonyesha wapi wanakwenza baada ya kuzingua mwanzoni.”

Chanzo: Mwanaspoti