Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Odegaard afichua siri ya mafanikio

Odegaard Ert.png Odegaard afichua siri ya mafanikio

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Arsenal Martin Odegaard amekiri kwamba Kocha Mikel Arteta ndiye aliyesababisha kiwango chake kuimarika kwa asilimia kubwa kutokana na mazoezi kila siku.

Kiungo huyo amemsifu kocha wake kutokana na mwenendo tangu alipokuwa chini ya kocha huyo Mhispania na ameonekana kubadilika baada ya kusota kwa muda mrefu.

Odegaard alikuwa kinara katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United kufuatia ushindi wa mabao 31 kwenye Uwanja wa Emirates.

Kiungo huyo amesema anajiona ni mchezaji wa daraja la juu kutokana na Arteta ambaye alimwamini na kumpa nafasi nyingi za kucheza.

“Kuna mambo mengi sana yametokea kwenye mechi zetu, sikuwahi kufikiria hata kidogo, wapinzani wakija na mbinu na mimi nakuja kwa utofauti mkubwa, nikisimama eneo sahihi naamini nitafanya jambo kwa ukubwa zaidi.

“Mpira unapokuwa karibu yangu naelewa ninachotakiwa kufanya. Mambo yanakuwa mengi tunapokuwa mazoezini, kocha mara nyingi anatoa amri na ina maana kubwa kwetu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live