Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Odegaard achekelea kuondoka Madrid

Martin Odegaard Kiungo wa Arsenal, Martin Odegaard

Mon, 16 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo wa Arsenal, Martin Odegaard amesema kuondoka Real Madrid na kujiunga na Arsenal ilikuwa uwamuzi sahihi baada ya kukipiga Santiago Bernabeu tangu alipokuwa na umri wa miaka 16.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway alitimka Hispania na kwenda London kwa uhamisho wa kudumu wa Pauni 30 milioni miaka miwili iliyopita baada ya mkopo kumalizika Arsenal.

Odegaard alikabidhiwa unahodha wa Arsenal Julai mwaka jana kutokana na mchango wake na kiungo muhimu katika kikosi cha kocha Mikel.

Kiungo huyo alicheza mechi 11 kwenye kikosi cha kwanza cha Madrid na alishindwa kufunga au kutengeneza asisti lakini akasisitiza alijifunza mambo mengi wakati alipokuwa akiishi Hispania.

“Mambo yalikuwa mazuri kwangu wakati nilipokuwa Madrid. Ilikuwa hatua nzuri, ingawa labda wengine wanaweza kufikiria vinginevyo,” alisema Odegaard.

“Nilijifunza mengi, nilipambana na niliweza kufanya mazoezi na baadhi ya wachezaji bora duniani. Lakini mwisho, nilifanya maamuzi sahihi kuondoka. Nilitaka kuendeleza soka langu na kukua zaidi.”

Kikosi cha Madrid kilisheheni mastaa wengi kama Luka Modric, Toni Kroos, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale wakati Odegaard anakipiga huko na alishindwa kutoboa kikosi cha kwanza. Hata hivyo, bado anaendelea kuipenda Madrid na kusisitiza ni klabu kubwa zaidi duniani; “Real Madrid ndiyo klabu kubwa zaidi duniani kila mtu anafahamu, hata kama Ronaldo, na Beckham wasingekuwepo kipindi kile.”

Kiwango bora cha Odegaard ilichangia Arsenal kumwongeza mkataba mpya wa muda wa miaka mitano ambao utamweka hadi mwaka 2028.

Arsenal ilikaribia kunyanyua taji la Ligi Kuu England msimu uliopita kabla ya kuboronga katika mechi tano za mwisho na kuipa mwanya Manchester City.

Chanzo: Mwanaspoti