Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Obi Mikel: Sijawahi kuona mchezaji mvivu kama Eden Hazard

John Obi Mikel Label Hard John Obi Mikel akimzungumzia Eden Hazard

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa Klabu ya Chelsea John Obi Mikel amefunguka mengi ambayo aliwahi kuyashuhudia alipokuwa Klabuni hapo hasa vile vya nyuma ya pazia.

Moja kati ya kubwa ambalo amelipasua kwenye mahojiano yake na Dubai Eye ni la Eden Hazard.

Kiungo huyo raia wa Nigeria amesema licha ya kuwa mshindi uwanjani mara kwa mara, Eden Hazard ni mchezaji mvivu kuwahi kumshuhudia kwenye maisha yake, amesema alikuwa hafanyi mazoezi kabisa.

“Hakuwahi kufanya mazoezi. Mchezaji mvivu zaidi kuwahi kumuona kwenye maisha yangu. Lakini ikifika wikendi, anafanya vizuri anakuwa nyota wa mchezo.”

Mikel na Hazard wameshinda mataji matano pamoja ndani ya Chelsea chini ya Makocha Jose Mourinho, Rafael Benitez, Guus Hiddink na Antonio Conte. Waliondoka Stamford Bridge kwa kufuatana, Mikel akiondoka 2017 huku Hazard akitimkia Real Madrid 2019.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live