Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nzoia Sugar waitaka Michuano ya CAF

Nzoia Sugar Nzoia Sugar waitaka Michuano ya CAF

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mkabaji wa Nzoia Sugar inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kenya Boniface Munyendo amesema malengo ya klabu hiyo ni kuona wanakuwa sehemu ya wawakilishi wa taifa la Kenya kwenye michuano ya CAF msimu ujao.

Munyendo amesema hayo katika kipindi hiki ambacho timu yake inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa KPL wakiwa na alama saba alama tano pungufu ya kinara na bingwa wa mtetezi wa taji hilo Tusker.

Sofapaka na KCB ni moja ya timu ambazo zimeonja maumivu ya Nzoia Sugar kwani wameweza kushinda mbili na kutoa sare moja.

“Msimu huu hatutaki kuzungumza mambo mengi, tunahitaji kuona tunafanya vizuri zaidi uwanjani, matendo yetu yajieleze”, alisema Munyendo kiungo ambaye kwa msimu huu amekuwa kwenye ubora mkubwa.

Mshindi wa Ligi ataenda kucheza michuano ya Shirikisho lakini mshindi wa kombe la Shirikisho atacheza shirikisho la CAF.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live